Thursday, April 15, 2010

MIJADALA MASWALI NA MAJIBU KUHUSU SHERIA YA KAZI

SWALI:
Hivyi ikitokea mwajiri kakulipa msharaha kimakosa (yani kazidisha amount fulani katika mshahara wako kwa mda wa zaidi ya miezi 2) je ni sahihi mshahara wako kushushwa tena kama hilo kosa lilikuwa la mwajiri. je sheria ya kazi inasemaje kuhusu hilo wanasheria tunaomba mtutafsirie.

MICHANGO/MAJIBU:

Hapa swali lako limekaa kimtego kidogo. Lakini kama nimekuelewa vizuri, unazungumzia makosa ya payroll tu. Na sio kwamba mwajiri amekupa kabisa barua ya increment then anataka kushusha mshahara after two months. Kama ni overpayments due to payroll errors, mwajiri anaruhusiwa kukukata hiyo overpaid amount provided that the total deductions does not exceed one quarter of your salary.

Section 28(5) of the ELRA 2004 states that; An employer shall not require or permit an employee to (a) repay any remuneration except for overpayments previously made by the employer resulting from an error in calculating the employee's remuneration.

So, deductions zinaruhusiwa kisheria kama kweli kuna kosa la overpayments.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
SWALI:
Je, ninaweza kuacha kazi in 24Hrs kutokana na mwajiri kutotimiza makubaliano?
Mimi nimekuwa katika ajira na mwajiri wangu mpya yapata mwaka sasa. Katika mkataba wa ajira, tulikubaliana mambo kadha wa kadha (mbali na mshahara), ni pamoja na marupurupu kwa ajili ya kodi ya nyumba, mawasiliano na usafiri.

Hata hivyo, tangu mwenzi wa kwanza katika kumtumikia, marupurupu hayo yameonekana kuwa ni hadithi tu, kila kukicha ni subiri na subiri. Mwaka waisha sasa. Binafsi, nahisi kutotendewa haki na kwa maana nyingine nachukulia suala hili ni mpango tu wa kuhujumu utendaji na ufanisi wangu katika kazi.

Baada ya kuwa nikifuatilia suala hili, pengine na hata kuonekana nakuwa bughudha, taratibu nilianza kuishiwa na hari ya kazi na pia kuanza kufikiria kutafuta ajira mpya.

Hivi punde nimepata wito kutoka kwa mwajiri mpya, ambaye agependa nijiunge naye mapema iwezekanavyo.

Swali langu la msingi ni je, naweza kuamua kuacha kazi kwa short notice? Moja pia kati ya makubaliano katika mkataba ni kutoa notice ya mwezi mmoja!

Naomba msaada kwa wenye kujua na kuwa na uzoefu na masuala haya ya haki za wafanyakazi na sheria kwa ujumla.

Ahsanteni

MICHANGO/MAJIBU:
Kwanza naomba uangalie vizuri mkataba wako na mwajiri kama unakipengele cha kuacha kazi, na kinasemaje???
Maana mikataba mingi ya kazi huwa inakipengele cha kuacha kazi kwa kutoa notice ya mwezi mmoja, na notice ya kuacha kazi masaa 24 kwa masharti kwamba inatakiwa kumlipa mwajiri wako mshahara wa mwezi mmoja.

Angalia vizuri mkataba wako naamini kipengele hicho huwa kinakuwepo.....kama kipengele hakipo, itakuwa ni vigumu kuacah kwa masaa 24, maana utakuwa huna mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, maana Mkataba ndio unakuwa kimbilio lako kwa wakati huo.....na inaweza kukufanya ukakosa haki zako nyingine.
..............................................................................
Kama nilivyosema hapo awali, mkataba unanitaka aidha kutoa notice ya mwezi mmoja and kama nitaamua kuacha kwa muda mfupi, nimlipe mwajili fedha taslimu inayolingana na mshahara wangu wa mwezi mmoja.

tatizo langu la msingi nililonalo ni kwamba, ikiwa na yeye hakuweza kutimiza makubaliano yaliyopo katika mkataba, ikiwa ni pamoja na kunilipa marupurupu niliyoyaainisha katika post yangu ya mwanzo, je naweza kuchukulia hicho kama kigezo na kuamua kubwaga manyanga?

Binafsi, nakuelewa sana unaposema mimi kukosa baadhi ya haki zangu, lakini naamini pia kuendelea kumtumikia na kuacha this other opportunity ni kuendelea kupoteza haki zangu zaidi.

tafadhali nishaurini. Najua kunaweza kuwa na wenzangu wengi tu ambao wamekumbana na ahadi za namna hii za kilaghai kutoka kwa waajiri ili mradi tu uwazalishie.

1 comment:

  1. nimefurahi sana kuingia katika sehemu hii ili nami nisaidiwe. SWALI LANGU NI JE NI VIGEZO VIPI VINATUMIWA KULIPA MTU ALIYEFANYA KAZI ZAIDI YA MUDA WA KAWAIDA WA KAZI, YAANI OVERTIME?...UNAKOKOTOAJE MALIPO YAKE. NAOMBA UNIJIBU KWA KUZINGATIA PANDE ZOTE ZA MUUNGANO YAANI TANZANIA BARA NA TANZANIA VISIWANI KAMA KUNA TOFAUTI KATI YA KUKOKOTOA MALIPO HAYA UKIWA BARA NA UKIWA VISIWANI. JE, NAWEZAJE KUPATA SHERIA HIZO?. NATANGULIZA SHUKRANI.

    ReplyDelete

MIJADALA MASWALI NA MAJIBU KUHUSU SHERIA YA KAZI

MY BLOG VISITORS COUNTER